pmbet

Mji wa kimkakati wa Somalia waangukia mikononi mwa Al-Shabab

Eric Buyanza

July 28, 2025
Share :

Wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shabab wameudhibiti mji wa kimkakati wa Maxaas katikati mwa Somalia siku ya Jumapili baada ya mapigano makali na jeshi na wanamgambo wa eneo hilo, duru za kijeshi zimesema. 

Kundi la Al Shabab lenye mafungamano na Al-Qaeda limechukua makumi ya miji na vijiji tangu lianze mashambulizi mapema mwaka huu, na kurudisha nyuma karibu mafanikio yote yaliyopatikana na serikali katika operesheni zake za kijeshi mwaka wa 2022 na 2023.

Katika taarifa, Al Shabab wamesema wameuchukua mji wa Maxaas, karibu kilomita 300 (maili 186) kutoka mji mkuu Mogadishu, ambao unachukuliwa kuwa kitovu cha kimkakati cha usafiri na usafirishaji katika eneo la kati.

Wanajeshi wa jeshi la taifa la Somalia wamethibitisha kutekwa kwa mji wa Maxaas, ingawa wamedai kuwa ilikuwa " mbinu ya kijeshi".

Mohamed Dahir, kamanda wa jeshi katika eneo hilo, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Al Shabab walishambulia kwa "mabomu na mamia ya wapiganaji waliokuwa na silaha nzito" mapema Jumapili.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet