pmbet

Mji wa kwanza duniani kuacha kutumia pesa taslimu

Eric Buyanza

November 17, 2026
Share :

Serikali ya Pakistan imetangaza mpango wa kuifanya Islamabad kuwa "mji mkuu wa kwanza duniani usiotumia fedha taslimu" na pia “mji wa kwanza nchini humo unaotumia mfumo wa malipo ya kidijitali.”
 

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya ndani Ijumaa (Novemba 13), serikali imeweka tarehe 31 Desemba kuwa tarehe ya mwisho ya utekelezaji wa mpango huo.
 

Hatua hii imelenga kuhakikisha kwamba kufikia tarehe hiyo, biashara zote na wafanyabiashara wote mjini Islamabad wanaunganishwa na mfumo wa malipo ya kidijitali.

 

Kwa mujibu wa Wizara ya mambo ya ndani, kikao muhimu kuhusu mradi huo ulioitwa kwa lugha ya kimombo "Cashless Islamabad" kiliongozwa na Waziri wa nchi anayeshughulikia Mambo ya ndani, Talal Chaudhry.

 

Talal Chaudhry alisema lengo ni kuhakikisha kuwa biashara zote za Islamabad zinaingia kwenye mfumo wa malipo ya kidijitali ifikapo Desemba 31.

 

Kwa mujibu wake, baada ya Novemba 30, fedha taslimu hazitakubaliwa tena katika idara yoyote ya Islamabad Capital Territory (ICT) na Mamlaka ya Maendeleo ya Jiji la Islamabad (CDA).
 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet