pmbet

Mjue Daulat Maharaj, ana mwaka wa 5 hajawahi kukaa

Eric Buyanza

June 20, 2026
Share :

Daulat Giri Ji Maharaj kutoka nchini India ambaye amepata umaarufu mkubwa duniani baada ya video zake kusambaa mitandaoni zikionyesha akifanya ibada ngumu ya kusimama bila kukaa wala kulala kwa miaka mitano mfululizo huku akiapa kufikisha miaka 12.
 

Yeye ni muumini wa mila ya kale ya Kihindu inayojulikana kama "Standing Babas" au Khadeshwari Tapasya (Toba ya Kusimama). Aliamua kuacha masomo yake ya chuo kikuu na kujitolea maisha yake yote kwenye ibada hii ngumu kwa lengo la kupata utakaso wa kiroho na kupata maono ya kimungu kutoka kwa Mungu Shiva (Mahadev).
 

Watu wengi hujiuliza jinsi anavyoweza kupumzika au kulala bila kukaa au kulala chini. Daulat Giri anatumia miundombinu maalum kama bembea ya kamba au machela ya kuning'inia. Wakati wa usiku au anapotaka kupumzika, anaegemeza kifua na mikono yake kwenye kamba hizo zinazomshikilia akiwa amesimama, huku miguu yake ikiwa bado imegusa chini, hivyo halali kitandani.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet