Mjue jamaa aliyemeza kijiko na akabaki nacho kooni kwa mwaka mzima
Eric Buyanza
February 24, 2024
Share :
Katika hali ya kushangaza mwaka 2017 huko nchini china kwenye Hospitali ya Xinjiang Meikuang, madaktari walimpokea mgonjwa wa ajabu aliyetambulika kwa jina la Zang.
Tunasema wa ajabu kwasababu mgonjwa huyo alikuwa amemeza kijiko kilichokuwa na urefu wa sentimita 20 na kikakwama kwenye koo lake.
Madaktari hao walipambana na kufanikiwa kukitoa.
Zang aliyekuwa na umri wa miaka 20 wakati huo, anasema kijiko hicho hakikumpa matatizo yoyote makubwa kiasi kwamba aliweza kumudu kuendelea na shughuli zake kwa mwaka mzima bila ya kuhisi maumivu yoyote.