pmbet

Mjue Lina, mwanamke mwenye uhusiano na wastaafu 7 na wote wanamhudumia

Eric Buyanza

June 15, 2024
Share :

Katika hali ya kushangaza mwanamke mmoja wa Colombia aliyefahamika kwa jina la Lina, amezua sintofahamu miongoni mwa jamii inayomzunguka baada ya kugundulika kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na wazee wastaafu 7, wengi wakisema hana mapenzi ya dhati na wazee hao bali yuko nao kwa ajili ya pesa.

Lina amekuwa gumzo nchini Colombia baada ya hadithi yake isiyo ya kawaida kuenea mtandaoni. 

Inaelezwa kuwa baada ya mfululizo wa mahusiano ya kimapenzi yenye kukatisha tamaa na kuumizwa na wanaume wa rika lake, msichana huyo aligundua mbinu ambayo ingempa utulivu wa moyo na wa kifedha kwa kuwalenga wazee wastaafu. 

Lina akakumbuka jinsi mume wa jirani yake (mzee) alivyokuwa akimsumbua kwa kumtongoza mara kwa mara, ndipo alipogundua kuwa atakuwa anatamaniwa na wazee, na wazee kawaida yao huwa wako tayari kutoa chochote ili wawe na wanawake kama wa umri wake.

Kwa hiyo alianza kwenda kwenye bustani na maeneo mengine ambayo wazee wapweke kwa kawaida hujumuika, na hapo ndipo alipowanasa wstaafu hao 7 ambao wote wanamsaidia kifedha.

Wazee hao Carlos, Simón, Jesus, Pablo, Manuel, na wengine wawili ambao hawakutaka kutaja majina yao, wote wanafahamiana na hawaoneani wivu. 

Wote wana jukumu la kulipia gharama za Lina na kumsaidia kazi za nyumbani kama (kusafisha nyumba, kufua, kupika n.k.) na wanashindana kumuonyesha mahaba.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet