Mjue mchinjaji wa serikali ambaye kila siku hupita kuziomba radhi familia
Eric Buyanza
February 22, 2024
Share :
Muhammad Saad Al-Beshi ni mchinjaji mkuu wa serikali ya Saudi Arabia ambaye huwakata vichwa kwa upanga hadharani wafungwa waliohukumiwa kifo.
Muhammad huwakata vichwa hadi watu saba kwa siku. Mwenyewe kwenye moja ya mahojiano aliyowahi kufanyiwa alisema hiviiii...
"Haijalishi kwangu: Wawili, wanne, 10 - mradi ninafanya mapenzi ya Mungu, haijalishi ni watu wangapi ninaowaua,"
Aliwahi kuambia BBC kuwa kila siku huzitembelea familia za wafungwa aliowachinja ili kuomba msamaha.
Muhammad analipwa mshahara wa Riyal 8,000 kwa mwezi (sawa na shilingi milioni 5.5 za kitanzania) na amefanya kazi hii tangu mwaka 1998.