Mjue mkazi wa Mumbai aliyeziba zaidi ya mashimo 6000 baada ya kifo cha mwanae
Eric Buyanza
March 23, 2024
Share :
Huko nchini India Julai 28, mwaka 2015, mkazi wa jiji la Mumbai aliyefahamika kwa jina la Dadarao Bhilhore alipoteza mtoto wake wa kiume Prakash, baada ya baiskeli aliyokuwa akiendesha kutumbukia kwenye shimo refu kwenye Barabara ya Jogeshwari-Vikhroli na kumsababishia kifo.
Tangu wakati huo, Bwana Bhilhore alianza kujaza mashimo yote kwenye barabara za jiji hilo ili kuzuia matukio kama hayo. .
Bhilore anasema hataki msafiri yeyote apoteze maisha kwasababu ya mashimo kama ilivyokuwa kwa mtoto wake Prakash.
Hadi kufikia mwaka 2020 alikuwa tayari ameshaziba mashimo 6,000
Mzee huyo Alisema hataacha kazi hiyo hadi aifanye India isiwe na mashimo.