pmbet

Mjue mke wa Rais aliyekimbia ndoa za utotoni

Eric Buyanza

May 19, 2026
Share :

Fatima Bio alikimbia nchini Sierra Leon mwaka 1996 alipokuwa na umriwa miaka 16 na kupata hifadhi jijini London, hii ni kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwanamke huyo anasimulia alikuwa karibu kuwa bibi harusi wa utotoni. Kufikia alipofikisha miaka 13, baba yake, mchimbaji wa almasi kutoka wilaya ya Kano, alikuwa tayari amepanga aolewe na mwanaume mwenye umri wa zaidi ya miaka 30 ambaye alikuwa akimfahamu kama baba tangu akiwa mtoto mdogo.
 

Mambo mengi yamebadilika tangu wakati huo. Katika miaka iliyofuata, alikuja kuwa muigizaji, kisha akakutana na mwanaume mmoja London alipokuwa akimhoji kuhusu Wasierra Leone wenye ushawishi wanaoishi ughaibuni, na baadaye wakafunga ndoa. Mwanaume huyo alikuwa Julius Bio, ambaye sasa ni rais wa Sierra Leone.
 

"Uingereza ilikuwa neema yangu kubwa. Nilipokwenda England, nilipata sauti yangu," alisema mke huyo wa rais. "Nilipata uhuru wangu, na ndipo nikaweza kujitetea mwenyewe. Na sasa ninaweza kupigania vijana wengi iwezekanavyo.”Alisema Fatima.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet