pmbet

Mjue mwanaume aliyekaa mafichoni miaka 55, kisa anaogopa wanawake!

Eric Buyanza

February 17, 2024
Share :

Mwanamume mmoja wa nchini Rwanda amedaiwa kujitenga na kuishi peke yake kwa miaka 55 kwa sababu ya hofu kubwa aliyonayo kwa wanawake.
 

Callixte Nzamwita, mwenye umri wa miaka 71, anadaiwa kwa miaka 55 aliishi mafichoni  ili kuepuka kukutana na wanawake.
 

Inasemekana Bw Nzamwita alianza kujitenga akiwa na umri wa miaka 16 na alikuwa akilala, kula na kupika katika eneo la makazi ya peke yake.
 

Kwa mujibu wa Bw Nzamwita alisema sababu ya kujifungia ndani na kuwa na uzio kwenye kijumba chake...ni kwa sababu anataka kuhakikisha hakuna mwanamke yoyote atakayemkaribia.
 

Kwa mujibu wa madaktari hali anayopitia Bw Nzamwita ni ugonjwa unaoitwa Gynophobia, ambao unamfanya mtu kuwa na hofu kubwa ya wanawake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet