pmbet

Mjue Pedro Lopez, muuaji hatari zaidi katika historia ya dunia

Eric Buyanza

May 6, 2026
Share :

Pedro Alonso López, anayejulikana pia kama "Monster of the Andes" (Mnyama wa Milima ya Andes), ni mmoja wa wauaji hatari zaidi katika historia ya dunia.
 

López aliwahi kukiri kuua zaidi ya mabinti wadogo 300 (wenye umri wa miaka 8 mpaka 12) nchini Colombia, Peru, na Ecuador kati ya miaka ya 1970 na 1980. Polisi walithibitisha vifo vya angalau watu 110 baada ya yeye mwenyewe kuwaongoza kwenye makaburi ya siri.

 

Mtu huyu hatari alikuwa akitumia mbinu ya kuwarubuni mabinti hao masokoni na maeneo mengine kwa kuwapa zawadi au ahadi feki, kisha kuwateka, kuwabaka, na baadae kuwanyonga.
 

Alikamatwa mwaka 1980 nchini Ecuador baada ya kushindwa kumteka msichana mmoja. Alihukumiwa miaka 16 jela, ambayo ilikuwa adhabu ya juu zaidi nchini Ecuador wakati huo.

 

Cha kushangaza ni kwamba aliachiliwa mwaka 1994 kwa "tabia njema" na kurejeshwa Colombia. Baada ya kukaa kwenye hospitali ya vichaa kwa muda, alitangazwa kuwa "mzima" na kuachiliwa huru kabisa mwaka 1998.

 

Tangu alipoachiliwa mwaka 1998, hajulikani alipo. Ingawa Interpol ilitoa kibali cha kumkamata tena mwaka 2002 kwa uhalifu mwingine, bado ni mtu anayetafutwa na wengi wanaamini anaweza kuwa bado yuko hai au alikufa bila watu kufahamu.
 

Maisha yake yamejaa ukatili uliopitiliza, na kuachiliwa kwake huru kunatajwa kama moja ya makosa makubwa zaidi ya mifumo ya sheria duniani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet