Mjue Rais aliyefariki akiwa ndani ya Mahakama
Eric Buyanza
July 26, 2025
Share :
Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi alifariki dunia tarehe 17.06.2019 akiwa ndani ya mahakama jijini Cairo wakati akisikiliza kesi iliyokuwa inamkabili.
Morsi alichaguliwa kidemokrasia na baadae kapinduliwa na jeshi mwaka 2013 baada ya kukaa madarakani kwa mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa Televisheni ya taifa ya nchi hiyo, Mohammed Morsi alianguka mahakamani wakati kesi yake ilipokuwa ikisikilizwa na kufariki.
Inaelezwa kuwa Morsi alikuwa amemaliza kujitetea akiwa katika chumba kilichozungushiwa vioo ndani ya mahakama na wakati wa utetezi wake alionya kuwa ana 'siri nyingi' na nzito ambazo angeweza kuzifichua, dakika chache baadae alianguka na kupoteza fahamu.
Televisheni ya taifa ilisema Morsi alikufa kabla hajapelekwa hospitali. Chama cha Morsi kiliilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kumuua.