Mjue shabiki wa Arsenal aliyemhadaa mkewe kwenye jina la mtoto
Eric Buyanza
March 19, 2024
Share :
Mwaka 2016 shabiki wa mpira wa miguu wa huko nchini Australia alifanikiwa kumhadaa mke wake na kumpa mtoto wao mpya jina 'LANESRA'.
Ilimchukua mke wa jamaa huyo miaka miwili kuja kugundua utapeli aliofanyiwa na mume wake.
UTAPELI GANI?
Jina hilo alilopendekeza jamaa wampe mtoto wao, lilikuwa jina la timu yake pendwa ya ARSENAL, alichofanya ni kugeuza maneno na kupata jina 'LANESRA'..linaandika gazeti la The Guardian la nchini Uingereza.