Mjue tajiri aliyeoa mwanafunzi, mwalimu na mkuu wa shule
Eric Buyanza
March 25, 2026
Share :
Kutana na mwanamume mmoja tajiri wa Saudi Arabia mwenye umri wa miaka 50 ambaye alifanya uamuzi wa ajabu uliozua gumzo mwaka 2012 kwa kuoa mwanafunzi, mwalimu na mkuu wa shule wote kutoka kwenye shule moja.
Inaelezwa kuwa ndoa za mwanaume huyo, ambaye hakutajwa jina na gazeti la Saudi la Okaz, zilifanyika kwa nyakati tofauti na zilisajiliwa kisheria, huku mwanamume akieleza kuwa kila ndoa ilikidhi matakwa ya kisheria na kidini.






