pmbet

Mjue Tshekedi Pitso, mfanyabiashara aliyezikwa akiwa ndani ya gari lake

Eric Buyanza

February 23, 2024
Share :

Aliyekuwa mwanasiasa na mfanyabiashara wa Afrika Kusini, "Tshekedi Pitso" alikuwa akilipenda sana gari lake aina ya Mercedes Benz kiasi cha kuomba azikwe nalo siku akifa.

Unaambiwa miaka miwili kabla ya kifo chake alikuwa akiwaambia ndugu zake jinsi anavyotaka kuzikwa siku akifa, na moja ya jambo lililowashangaza ndugu hao ni pale alipowaambia anataka kuzikwa na gari lake pendwa. 

Siku ya maziko yake wanakijiji alichozaliwa walibaki na mshangao waliposhuhudia mwili wa mfanyabiashara huyo ukiingizwa kaburini ukiwa ndani ya gari na mwenyewe akiwa amekaa kama anaendesha.

Mfanyabiashara huyu alikuwa na magari mengi lakini hilo ndilo gari alilokuwa akilipenda zaidi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet