Mjue wakili 'Feki aliyefanikiwa kushinda kesi 26
Eric Buyanza
May 25, 2024
Share :
October mwaka jana 2023 huko nchini Kenya, zilizuka story zilizokuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya polisi kutangaza kumshikilia mwanaume mmoja 'Wakili feki' aliyekuwa akifanya kazi za kisheria (wakili) akitumia jina la Brian Mwenda (sio jina lake).
Jamaa huyo alikuwa akitumia utambulisho wa wakili halisi aitwae Brian Mwenda Ntwiga.
Gazeti la Citzen liliripoti kwamba, jamaa huyo akiwa anatumia utambulisho ambao sio wake alifanikiwa kushinda kesi 26, alizoziwasilisha mbele za Mahakimu, Majaji wa Mahakama ya Rufaa, na majaji wa Mahakama Kuu.
Hata hivyo kulizuka sintofahamu miongoni mwa wananchi nchini humo huku wengi wakionekana kumtetea wakidai afutiwe mashataka kwani ni kijana mpambanaji aliyevumbua namna ya kujipatia riziki.