Mkaa huondoa sumu ya pombe, na kukata pombe mwilini - Mtaalam
Eric Buyanza
August 20, 2024
Share :
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Huduma ya kwanza wa Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA) Moteswa Meda, wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari Tanzania (JOWUTA) mafunzo yaliofunguliwa na Mtendaji mkuu wa OSHA, Hadija Mwenda, makao ,makuu ya OSHA.
Moteswa alisema mkaa ni kitu muhimu kukaa nacho nyumbani kwa kuwa kina msaada mkubwa kwa Binadamu hasa katika eneo la uokozi.
Alisema kwa mtu aliyelewa kwa kiwango kikubwa anaweza kurejea kwenye hali yake ya kawaida kwa muda mfupi sana endapo atatafuna mkaa, unafanya kazi kwenye kuondoa sumu kiwango cha pombe mwilini.
“Mkaa uondoa sumu ya pombe Mwilini kwa walevi. Mkaa unaweza kuokoa maisha ya mtu aliyekunywa sumu kama mtu amekunywa sumu ya aina yoyote au idadi kubwa ya vidonge ambapo kinachofanywa sio kumpa maziwa au maji badala yake ni kumpa mkaa atafune kama anaweza kutafuna ” alisema Meda.
Alisema mtu anapokunywa sumu au kilevi apondewe mkaa hadi uwe na unga kumeza bila maji mtu aliyekunywa sumu aina yoyote au vidonge anatakiwa asipewe Kimiminika akipewa anaongezewa uharaka wa kufa maana anaenda kuipa nguvu sumu isambae kwa haraka Mwilini.
“Mkaa ukiingia tumboni kwa wingi unakwenda kuifyonza ile sumu iliyopo mwilini na kumpunguzia mtu hatari ya kufa, hata hivyo pamoja na kutoa huduma hiyo ya kwanza inapaswa kuhakikisha aliyekunywa sumu anakimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi ” alisema.
TM