Mke wa Kashogi apata hifadhi Marekani
Eric Buyanza
December 22, 2023
Share :
Hanan Elatr ambaye ni mke wa Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari aliyeuawa akiwa katika Ubalozi mdogo wa Saudia Mjini Istanbul mnamo Oktoba 2018, amepewa Hifadhi ya kisiasa rasmi nchini Marekani.
Taarifa za kijasusi za Marekani zilidai Saudi Arabia ndiyo iliyohusika na mauaji hayo kutokana na mwandishi huyo kuwa mkosoaji wa Utawala wa Taifa hilo.
Hanan ambaye alikimbilia Marekani kuomba hifadhi Agosti 2020 kutokana na kuhofia usalama wake amesema...... "Tumeshinda, walichukua maisha ya Jamal na kuharibu maisha yangu....ingekuwa hatari kiusalama kurudi Misri au Falme za Kiarabu nilipoishi kwa zaidi ya miaka 25."