Mke wa Mchezaji afariki dunia akiwa anamuokoa mtoto wake.
Joyce Shedrack
June 29, 2026
Share :
Mchezaji wa klabu ya Marítimo de La Guaira, Héctor Bello, amempoteza mke wake ambaye kwa ujasiri wa kipekee alijitoa mhanga kuokoa maisha ya binti yao kwa kumkinga kwa mwili wake chini ya vifusi vilivyoanguka kwenye tetemeko kubwa lililotokea Nchini Venezuela.
"Nitamsimulia hadithi ya jinsi ulivyomuokoa, mpenzi wangu, jinsi ulivyotoa maisha yako kwa ajili ya binti yetu, jinsi ulivyokuwa mwanamke jasiri ambaye hakuwahi kumuacha peke yake, hata ulipokuwa unatoa pumzi yako ya mwisho."
“Umetuacha tupambane na vita hii peke yetu. Nitamuambiaje binti yetu kwamba ulitoa maisha yako ili kuokoa yake, na kwamba mimi sikuwepo kufanya chochote?”
"Binti yangu na shangazi yake wanaendelea vizuri. Hawataruhusiwa kutoka hospitalini leo wataendelea kubaki hospitalini. Asanteni sana kwa kunisapoti na kunipa nguvu katika kipindi hiki cha maumivu makubwa sana," Amethibitisha nyota huyo kuwa binti yake anaendelea vizuri.





