pmbet

Mke wa Roma abadilisha jina siyo Mrs Roma tena.

Joyce Shedrack

October 18, 2024
Share :

Baada ya Rapa maarufu Roma Mkatoliki kuchapisha picha na video kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na mtoto wa kike na kuandika maneno ambayo yamepelekea watu wengi kuamini kuwa ni mtoto wake aliyempata akiwa nchini Marekani mke wa msanii huyo ambaye Instagram alikuwa anatumia jina la Mrs Roma amebadili jina hilo kwenye mtandao huo na kujiita jina lake halisi.

Mke wa Msanii  huyo ambaye alitimkia Nchini Marekani kwa zaidi ya miaka mitano tangu mwaka 2019 ametoka kwenye kujiita Mrs Roma mpaka kujiita jina lake halisi Nancy Daniel jambo ambalo limezua sintofahamu kuhusu ndoa ya wawili hao.

 

Wawili hao walifunga ndoa yao tangu mwaka 2016 na wamebarikiwa kupata watoto wawili mmoja wakiume mwengine wakike.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet