pmbet

Mke wa zamani wa Chivayo kusimamia mirathi

Sisti Herman

November 6, 2026
Share :

 

Mke wa zamani wa mfanyabiashara wa Zimbabwe, marehemu  Wicknell Munodaani Chivayo, na dada yake wamekubaliana kusimamia kwa pamoja mirathi ya marehemu, huku wakiweka masharti ya uwazi katika usimamizi wa mali, madeni na masilahi ya watoto wake wawili.

Sonja Louise Madzikanda na Esther Chivayo walitia saini hati ya makubaliano mjini Harare, Zimbabwe, Novemba 3, 2026, wakieleza namna wanavyokusudia kushirikiana katika kusimamia mali za marehemu.

Makubaliano hayo hayamaanishi tayari wameteuliwa rasmi kuwa wasimamizi wenza wa mirathi, bali uteuzi huo unahitaji kufuata taratibu za kisheria na kuthibitishwa na mamlaka husika kwa mujibu wa sheria.

Katika barua kwa Msajili wa Mirathi, wakili wa Madzikanda, Rungano Mahuni wa Mahuni Gidiri Law Chambers, amesema wahusika wamefikia mwafaka baada ya mashauriano.

“Tuna furaha kuwajulisha kuwa, kufuatia mashauriano kati ya wahusika, makubaliano yamefikiwa ya kuwateua Sonja Louise Madzikanda na Esther Chivayo kuwa wasimamizi wenza wa mirathi hiyo,” amesema Mahuni.

Kwa upande wa mawakili wa Esther, Caleb Mucheche and Partners, wamesema yeye ni dada wa marehemu na ndugu yake wa karibu, hivyo ushiriki wake unalenga kulinda masilahi ya familia, hususan watoto wawili walioachwa na marehemu, na kuepusha gharama za kumteua msimamizi mwingine wa kujitegemea.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet