Mkimtaka vunjeni benki
Sisti Herman
March 1, 2024
Share :
Rais wa klabu ya Napoli ya ligi kuu Italia De Laurentiis amethibitisha kuwa kama klabu vigogo barani Ulaya watahitaji saini ya mshambuliaji wao kinara Victor Osimhen lazima watoboke mkwanja mrefu sana ili kuuvunja mkataba wake.
βKuna kipengele katika mkataba kinaruhusu mauzo ya Victor Osimhen japo ni kwa kiwango cha juu sana, Baadhi ya wachezaji hukaa Napoli kwa miaka mingi ... wengine wanasakwa na PSG, Arsenal, Man City au Chelsea, Ni ngumu kuwaweka wachezaji Napoli haswa wanapotakiwa na vilabu hivi tajiri vya Ulaya" alithibitisha Rais huyo.
Kifungu cha kununua mkataba wa Osimhen kitakuwa tayari kutumika kuanzia majira ya kiangazi 2024 na kinatajwa kuanzia kiasi cha Euro milioni πππ hadi Euro milioni πππ.