"Mkitaka nibaki nipeni nyota wawili", Tuchel aimbia Bayern Munich
Eric Buyanza
May 17, 2024
Share :
Kocha wa Bayern Munich, Thomas Tuchel ameitaka klabu hiyo kumhakikishia itasajili wachezaji wawili nyota anaowataka kabla hajakubali kusaini mkataba mpya utakaomfanya asalie klabuni hapo.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 siku chache zilizopita amekuwa kwenye mfululizo wa vikao vya kumshawishi asaini mkataba mpya.
Tuchel ameiambia klabu hiyo anataka imsajilie wachezaji ambao amekuwa akiwaomba kwa muda mrefu.