Mkongo mwimgine atua Tabora
Sisti Herman
January 21, 2024
Share :
Klabu ya Tabora United imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo wa ulinzi, Nelson Omba Munganga ‘The Beast’ kutoka klabu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Munganga amewahi kuitumikia klabu ya AS Vita Club akiwa nahodha wa kikosi hicho na kufanikiwa kushinda tuzo ya kiungo bora kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mnamo msimu wa 2018/2019.
Amewahi pia kuitumikia klabu ya Magreb Fes inayoshiriki Ligi Kuu Morocco pamoja kuichezea timu ya Taifa ya Congo kwa nyakati tofauti.
Huu unakuwa usajili wa 3 kwa Nyuki hao wa Tabora kwenye dirisha dogo baada ya Patrick Lembo Anfumu na Kikwama Glody Mujinga.