Mkongwe Gullit ashindwa kuelewa: Mbappé anakosaje Ballon d’or!!
Eric Buyanza
November 26, 2026
Share :

Gwiji wa zamani wa soka wa Uholanzi na mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or mwaka 1987, Ruud Gullit, ameibua mjadala mkubwa katika ulimwengu wa soka baada ya kuonekana kushangazwa kwamba inawezekanaje Kylian Mbappé hajashinda Ballon d’Or mpaka leo akiwa anaenda kutimiza miaka 28!
"Inawezekanaje kwamba Kylian Mbappé anatimiza miaka 28 mwezi ujao, huku akiwa hajashinda tuzo hata moja ya Ballon d'Or? Hii inawezekanaje?! Nahitaji maelezo, kwa sababu jamaa amekuwa mfungaji bora katika kila mashindano makubwa kila mwaka." alisema mkongwe huyo.
Kauli hiyo ya Gullit imezua mjadala mpana miongoni mwa wachambuzi na mashabiki wa soka. Licha ya Mbappé kuwahi kuingia kwenye orodha ya wanaowania tuzo hiyo mara tisa na kumaliza katika nafasi ya pili mwaka 2026 pamoja na nafasi ya tatu mwaka 2023, bado hajafanikiwa kuibeba.
Baadhi ya wadau wanaamini kuwa kikwazo kikubwa kwa nyota huyo ni kukosa mataji makubwa ya pamoja kama Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) katika misimu ya hivi karibuni, jambo ambalo mara nyingi huzingatiwa sana na wapiga kura wa tuzo ya Ballon d'Or mbali na idadi ya mabao.





