Mkosoaji wa Serikali afariki Rwanda
Sisti Herman
December 29, 2023
Share :
Mkosoaji wa Serikali ya Rwanda, Anne Rwigara (41) amefariki Dunia baada ya kudaiwa kulalamikia maumivu ya tumbo kwa saa 8 yaliyopelekea viungo vyake vya mwilini kushindwa kufanya kazi.
Anne ni binti wa aliyekuwa Mfanyabiashara maarufu nchini Rwanda, marehemu, Assinapol Rwigara na dada wa Diane Rwigara ambaye aliwania Urais dhidi ya Rais Paul Kagame mwaka 2017.
Anne na mama yake, Adeline Rwigara walikaa gerezani kwa mwaka mmoja kwa tuhuma za kukwepa kulipa Kodi na Makosa ya Uchaguzi ambapo Mamlaka ya Mapato Rwanda ilisema familia ya Rwigara inadaiwa Dola Milioni 6.7 za kodi na hivyo Serikali ilifunga biashara ya familia na kufungia akaunti zao za benki.