pmbet

Mkuu wa Chuo atimuliwa baada ya kurekodi video za ngono na mkewe

Eric Buyanza

December 29, 2023
Share :

Chansela wa chuo kikuu cha Wisconsin nchini Marekani Bwana Joe Gow amefutwa kazi wiki hii baada ya kuchapisha video za ngono akiwa na mkewe mtandaoni.
 

Bodi inayosimamia vyuo vikuu nchini humo iliamua kwa kauli moja kumfukuza kazi Bwana Gow, ambaye amekiongoza Chuo hicho tangu mwaka 2007.

Karen Walsh, mkuu wa bodi, ambayo inasimamia vyuo vikuu 13 alisema katika taarifa kwamba bodi "imeshtushwa na kuchukizwa na matendo yake.
 

Katika mahojiano jana Bw. Gow na mkewe Bi. Carmen Wilson walisema ni makosa kwa chuo kikuu kuwaadhibu kutokana na video hizo, wakisisitiza kuwa kufanya hivyo kunakiuka haki zao za uhuru wa kujieleza.
 

Bw. Gow, 63, alisema yeye na mke wake, 56, wametengeneza video za ngono pamoja kwa miaka mingi lakini wameamua hivi majuzi kuziweka hadharani kwenye tovuti za pono.
 

Kwa mujibu wa Bwana Gow na mkewe hawakuwahi kutaja chuo kikuu au kazi zao kwenye video hizo ambazo zimeangaliwa na maelfu ya watazamaji na kupata maelfu ya maoni.
 

Wanandoa hao pia wametengeneza mfululizo wa video ambapo wanapika chakula na waigizaji wa ponografia na kisha kufanya ngon*

Jay Rothman, rais wa Chuo Kikuu cha Wisconsin amesema Bw. Gow amekisababishia chuo hicho madhara makubwa.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet