Mkuu wa Majeshi ahukumiwa jela miaka 5.
Sisti Herman
June 16, 2024
Share :
Jenerali Sadiba Koulibaly, Mkuu wa Majeshi mstaafu wa Guinea, amehukumiwa miaka mitano jela akituhumiwa kwa kutoroka pamoja na kuacha kazi akiwa nje ya nchi.
Juni 4 Sadiba Koulibaly alikamatwa na walinzi wake sita sababu kubwa ikiwa ni kusafiri nje ya Nchi bila idhini ya wakubwa wake.
Koulibaly baada ya kukamatwa na hatia mara moja alishushwa cheo na kuwa Kanali kabla ya kuondolewa katika jeshi la Guinea kwa kuhatarisha usalama wa nchi ,utovu wa nidhamu, kutoroka.