Mkuu wa majeshi Israel aapa "Shambulizi la Iran litajibiwa"
Eric Buyanza
April 16, 2024
Share :
Mkuu wa majeshi ya Israel Herzi Halevi ameapa kuchukua hatua za kulipiza kisasi dhidi ya Iran baada ya shambulizi lake la mwishoni mwa wiki. Iran ilirusha zaidi ya makombora 300 na droni kuelekea Israel Jumapili usiku.
Akitembelea kambi ya anga ya Nevatim, ambayo iliharibiwa kidogo na shambulio la Iran, mkuu wa jeshi la Israel, Herzi Halevi, aliwaambia wanajeshi wa jeshi la anga kwamba hatua ya Iran kurusha msururu wa makombora haiwezi kuachwa kupita bila kujibiwa.
Iran ilifanya shambulizi lake ambalo halijawahi kushuhudiwa, kulipiza kisasi kwa shambulio baya dhidi ya ubalozi wake mjini Damascus, ambalo linadaiwa kufanywa na Israel.
Viongozi wa dunia wameelezea hofu kwamba sasa kuna uwezekano wa vita vya wazi zaidi kati ya mahasimu hao wa muda mrefu na ghasia zinazotokana na vita vya Gaza kuenea zaidi.