pmbet

Mkuu wa majeshi Marekani Jenerali Randy George afutwa kazi

Eric Buyanza

April 3, 2026
Share :

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth amemfuta kazi mkuu wa majeshi Jenerali Randy George, pamoja na makamanda waandamizi wa jeshi kwa mujibu wa vyombo vya Habari nchini Marekani.

 

Hatua hii inajiri wakati huu Marekani na Israeli zikiendelea kutekeleza mashambulio mazito nchini Iran kulenga kituo cha muda cha utafiti kuhusu makubwa jijini Tehran, lakini pia kushambulia daraja linalotumiwa na raia na kiwanda cha chuma.

 

Mashambulizi haya yanakuja baaada ya rais Donald Trump kuonya kuwa Iran itashambuliwa na kuharibiwa kabisa, iwapo haitakubali mkataba wa kusitisha vita vinavyoendelea.
 

Rais Trump, kupitia mitandao yake ya kijamii, amesema jeshi la Marekani hata halijaanza kuharibu kabisa miundo mbinu ya Iran inayosalia, huku akisisitiza kuwa utawala mpya unafahamu kinachotakiwa kufanyika haraka.

 

Licha ya mashambulizi hayo, Iran nayo imeonya kuwa, vita vitaendelea hadi pale maadui wake ambao ni Marekani na Israeli, watakavyojisalimisha.

 

RFI

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet