Mkuu wa Mkoa akerwa kukosa huduma saa 3 hospitali
Sisti Herman
August 13, 2025
Share :
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amechemka hadharani kutokana na kile alichokiita huduma za aibu katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa Mawenzi na kumwagiza Katibu Tawala wa Mkoa, kufanya uchunguzi wa kina utendaji wa hospitali hiyo.
Akizungumza Agosti 12, 2025 katika kikao cha tathmini ya hali ya lishe kwa mwaka 2024/25, Babu alifichua tukio lililomkera binafsi alipowasili hospitalini humo, akiwa na mtoto wake aliyekuwa na dalili za degedege, lakini akakaa zaidi ya saa tatu bila kupatiwa huduma yoyote ya dharura.
Kwa sauti ya kuonesha mshangao na hasira, ameeleza kuwa aliwasili hospitalini akiwa amevaa kanzu na kofia, hivyo wahudumu hawakumtambua kama Mkuu wa Mkoa.
"Huduma pale ni za kusikitisha. Nilimpeleka mwanangu kwa dharura, lakini nilikaa naye muda mrefu bila msaada wowote. Wataalamu walikuwa wananitazama tu".