pmbet

Mkuu wa Mkoa kutoa mkate wa siagi kwa wafanyakazi

Eric Buyanza

May 6, 2024
Share :

Mkuu wa Mkoa wa kusini Unguja Visiwani Zanzibar, Ayoub Mohammed Mahamoud, ametangaza kuwapatia Wafanyakazi wa Ofisi hiyo chai ya asubuhi ikiwa na kitafunwa cha mkate wenye siagi kuanzia leo Jumatatu Mei 06, 2024 ili kupunguza wafanyakazi kuzurura saa za kazi, kuongea na simu mara kwa mara pamoja na kutoka nje kwenda kununua urojo. 

Ayoub aliyasema hayo jana wakati akifungua kampeni ya ‘Amshaamsha Kusini’ ikiwa na mahususi kwa watumishi wa serikali lengo likiwa ni kutokomeza uchelewaji makazini, kuzurura muda wa kazi na matumizi ya simu vitu ambavyo amesema haridhishwi navyo kwani vinachelewesha maendeleo ya wananchi ambapo amesisitiza kuwa gharama zote za chai na vitafunwa zitakuwa zikitoka kwenye mshahara wake yeye Mkuu wa Mkoa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet