pmbet

Mkuu wa Mkoa wa Iringa atangaza kugombea Ubunge

Sisti Herman

May 19, 2025
Share :

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba, ametangaza rasmi dhamira yake ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao, akisema sasa ni muda wa kuwatumikia Wananchi kwa ukaribu zaidi kupitia nafasi ya uwakilishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingawa bado hajaweka wazi atagombea Jimbo lipi.

 



Serukamba amesema hayo wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, kilicholenga kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.

“Mimi leo nadiriki kusema nadhani hii ni Halmashauri yangu ya Mkoa ya mwisho na Mimi nimekata shauri namuonea wivu Kaka yangu Lukuvi kukaa Bungeni muda mrefu na Mimi nataka niende hukohuko, na nina uhakika nitashinda huko ninakoenda, nawashukuru sana na wale wote mnaokwenda kugombea nawatakia kila la kheri “

pmbet

pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League

pmbet
pmbet