pmbet

Mkuu wa Polisi ahukumiwa kifo kwa kuua mwandamanaji

Eric Buyanza

March 28, 2024
Share :

Mahakama ya Iran imemhukumu kifo mkuu wa polisi Jafar Javanmardi baada ya kushtakiwa kwa kumuua mtu wakati wa maandamano makubwa mwaka 2022, vyombo vya habari vya ndani viliripoti Jumatano.
 

Javanmardi amehukumiwa kifo “kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu ya kulipiza kisasi, inayojulikana kama ‘qisas sharia’, kwa shtaka la mauaji ya kukusudia,” wakili wa familia ya mwathirika, Majid Ahmadi, aliliambia gazeti linalotetea mageuzi la Shargh.
 

Mwandamanaji, Mehran Samak, mwenye umri wa miaka 27, alifariki kutokana na majereha aliyoyapata baada ya kupigwa risasi wakati wa maandamano katika mji wa kaskazini wa Bandar Anzali tarehe 30 Novemba, mwaka 2022.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet