Mkuu wa Wilaya aagiza wanafunzi wazururaji wakamatwe
Eric Buyanza
March 28, 2024
Share :
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Kissa Kasongwa amewaagiza watendaji wa kata, mitaa na vijiji wilayani hapa kuwakamata wanafunzi ambao wanazurura mitaani wakati wa masomo, ili kukabiliana na tatizo la utoro pamoja na ukatili wa kijinsia.
“Mtoto atakayeonekana anazagaa wakati wa masomo achukuliwe, atafutwe mzazi wake na mzazi wake awajibishwe na jamii husika kwa sababu haiwezekani watoto tukawapoteza, watoto kwenye utoro wanafanyiwa vitu vibaya sana kuna mambo mengi yanatokea huko mtaani lazima tuwalinde watoto wetu,’’ amesema Kasongwa.