pmbet

Mlemavu wa macho aenda jela kwa kushika maumbile ya Binti wa miaka 14

Eric Buyanza

November 22, 2024
Share :

Mwanaume mmoja mwenye ulemavu wa macho huko Chipata nchini Zambia amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kwa kushika matiti ya msichana wa miaka 14.

Abraham Khondowe mwenye umri wa miaka 43, wa Kitongoji cha Walela, aligusa matiti na makalio ya binti wa jirani yake.

Wakati wa kesi katika Mahakama ya Chipata, msichana huyo, mwanafunzi wa darasa la 7, alisema tukio hilo lilitokea wakati wazazi wake wote wawili walipokuwa kwenye safari ya kikazi nchini Malawi.

Mahakama iliambiwa kuwa Bwana Kondowe alifanya majaribio ya kulala na Binti huyo kabla ya kutenda kosa hilo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet