pmbet

Mmarekani aenda jela miaka 30 kwa kusafirisha dawa za kulevya

Eric Buyanza

August 31, 2024
Share :

Raia wa Marekani Brandon Summerlin, amehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina Mescaline zenye uzito wa gramu 56.04 alizoziagiza kutoka nchini Peru. 
Aidha, raia huyo Summerlin katika utetezi wake aliieleza mahakama kuwa dawa hizo alikuwa akizitumia kama kiburudisho cha kuweza kumsaidia kupumzika.

Hukumu hiyo, imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Fahamu Kibona wa mahakama hiyo, baada ya kupitia sheria za dawa za kulevya, ushahidi, vielelezo na utetezi wa mshtakiwa.

Hakimu Kibona amesema upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi tisa na vielelezo saba, ambapo upande wa mashtaka uliweza kuthibitisha bila kuacha shaka lolote dhidi ya mashtaka yaliyokuwa yakimkabili mshtakiwa, kwa hiyo Summerlin amepatikana na hatia.

"Nimezingatia maoni ya upande wa mashtaka kuhusu athari za dawa za kulevya kiafya, kijamii, kiuchumi na kimataifa pamoja na utetezi wa mshtakiwa, mshtakiwa utatumikia kifungo cha miaka 30 jela," amesema Kibona

Pia, Hakimu Kibona ametoa amri kwamba kwamba kielelezo cha dawa hizo kiharibiwe kwa mujibu wa sheria ya dawa za kulevya na pia rufaa iko wazi kwa upande ambao haujaridhika.

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet