Mmiliki mpya Man United kumsogeza Olise Old Trafford
Eric Buyanza
January 4, 2024
Share :
Mchezaji wa Crystal Palace Michael Olise anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji wa kwanza kusajiliwa na Sir Jim Ratcliffe katika klabu ya Manchester United.
Ratcliffe, ambaye alinunua hisa za wachache za Mashetani Wekundu kwa pauni bilioni 1.3, yuko tayari kuvunja mkataba wa Olise Januari hii.