pmbet

Mmoja ajeruhiwa kwenye ajali ya viongozi wa Azam FC

Sisti Herman

May 16, 2024
Share :

Klabu ya Azam imethibitisha kuwa viongozi wao wa idara ya masoko na mauzo wamepata ajali alfajiri ya leo katika eneo la Magunike, Dumila mkoani Morogoro, ilipokuwa safarini kuelekea Mwanza ambapo klabu hiyo itacheza na Coastal Union kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB.

Ndani ya gari hilo binafsi kulikuwa na watu watatu, meneja wa idara, Tunga Ally na wasaidizi wake wawili, Ayubu Shelukindo na Venock Mkisi.

Meneja Tunga Ally aliyekuwa akiendesha, ndiye aliyeathirika lakini wengine waliobaki walitoka salama salimini.

Kwa msaada mkubwa wa jeshi la polisi, majeruhi alipelekwa hospitali ya Dumila na kupatiwa matibabu ambapo sasa anaendelea vizuri.

"Poleni sana timu yetu ya masoko na tunamwomba Mwenyezi Mungu amjalie afya njema majeruhi, Tunga" ilisema sehemu ya taarifa yao kwa kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet