pmbet

Mnaotaka lifti tusameheane tu au lipeni, mafuta ni ghali

Eric Buyanza

April 1, 2026
Share :

Bei ya Mafuta ya Petroli imepanda kwa kiwango kikubwa ambapo kwa Jiji la Dar es Salaam imepanda kutoka kiasi cha Sh. 2,864 kwa Lita na sasa imefikia kiasi cha Sh. 3,820 kwa Lita.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeeleza kupanda kwa bei hiyo kumetokana na mabadiliko ya soko la kimataifa, likiwemo ongezeko la bei ya mafuta ghafi na changamoto za usafirishaji. 

Kutokana na ongezeko hilo la kiasi kuwa kubwa, kuna haja ya wanaoomba lifti kwa marafiki zao nao kuchangia pesa kidogo ili kupunguza gharama za mafuta.

Hali ya kisiasa na kiusalama inayoendelea katika baadhi ya mataifa duniani, imechangia kuvuruga upatikanaji na usambazaji wa mafuta katika masoko mengine ya kimataifa.

Kwa mujibu wa EWURA, gharama za uagizaji na usafirishaji zimeongezeka, zikichangiwa pia na kupanda kwa gharama za bima ya meli pamoja na ucheleweshaji wa mizigo. Hali hii imepelekea bei za rejareja kupanda katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, ambako bei mpya zimeanza kutumika rasmi kuanzia leo Aprili Mosi mwaka huu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet