Mnapoteza muda wenu bure, Museveni aiambia Marekani
Eric Buyanza
January 11, 2024
Share :
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa majaribio ya mataifa ya nje ya kuishawishi nchi hiyo ni ya bure, hii ni zaidi ya wiki moja baada ya nchi yake kuondolewa kutoka kwenye mpango maalum wa kibiashara kati ya nchi za Afrika na Marekani baada ya Uganda kupitisha sheria yenye utata dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.
Sheria hiyo inaweka adhabu ya kifo kwa baadhi ya vitendo vya wapenzi wa jinsia moja.
"Kwa sasa, wale wanaotuwekea vikwazo, wanapoteza muda wao. Na hatupaswi kuwa na wasiwasi kuhusu hilo," Rais Museveni alisema katika hotuba yake ya kitaifa siku ya Jumanne.
"Tunachopaswa kuzingatia ni kupambana na ufisadi miongoni mwetu. Haya ndiyo matatizo halisi. Si shinikizo la nje, kwa sababu hilo halina maana," aliongeza.
Bw Museveni pia alisema kuwa Uganda itafanya biashara na washirika wa kimataifa ambao "wanaiheshimu".
BBC