Mnigeria asiyeamini mungu apunguziwa kifungo
Eric Buyanza
May 14, 2024
Share :
Mubarak Bala, Mnigeria asiyeamini kuwa kuna Mungu ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 24 jela kwa makosa yanayohusiana na kukufuru mwaka 2022, amepunguzwa kifungo hicho hadi miaka mitano baada ya kukata rufaa.
Kulingana na wakili wa Bala, James Ibori, jopo la majaji watatu katika jimbo la Kano liliamua kwamba hukumu ya awali ilikuwa "kali sana" na kinyume na vifungu vya sheria".
Bala, ambaye amekuwa gerezani kwa miaka minne, kesi yake ilizua hasira kwa baadhi ya mataifa alipokamatwa mwaka wa 2020.
Kundi la Waislamu lilikuwa limewasilisha ombi kwa mamlaka likimtuhumu Bala kwa kuchapisha ujumbe wa kukashifu Uislamu kwenye mitandao ya kijamii.
Baadaye alikiri mashtaka yote 18 na akahukumiwa kifungo cha miaka 24 jela na mahakama kuu katika jimbo la Kano kaskazi mwa Nigeria, lenye Waislamu wengi.
Kumekuwa na mashinikizo ya kutaka kuachiwa kwa Bala, kuzuiliwa kwake kumezua hofu kuhusu uhuru wa kujieleza nchini Nigeria.
BBC