Mnyama ashinda 2-1 'Pre Season' Misri
Sisti Herman
July 28, 2024
Share :
Klabu ya Simba imeshinda magoli 2-1 dhidi ya klabu ya Telecom Egypt ya Misri kwenye mchezo wa pili wa maandalizi ya msimu (Pre Season) uliochezwa Ismailia nchini Misri.
Kwenye mchezo huo magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji vijana Valentino Mashaka aliyefunga goli la kusawazisha dakika ya 63 baada ya Telecom kutangulia na Ladack Chasambi dakika ya 88.
Huo ni mchezo wa pili wa Simba baada ya wiki iliyopita kushinda 3-0 dhidi ya Canal SC kwenye mchezo wa kwanza wa 'Pre Season'.