Mnyama kujipima nguvu na timu ya Saudia Arabia leo.
Joyce Shedrack
August 20, 2025
Share :
Klabu ya Simba inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki siku ya leo saa 11:30 jioni dhidi ya timu Al Zulfi ya nchini Saudi Arabia.
Simba ambayo imeweka kambi ya maandalizi ya Msimu mpya Jijini Cairo Nchini Misri itajipima nguvu na Al Zulfi inayoshiriki ligi daraja la pili Nchini Saudia Arabia.