Mo afanya balaa Msimbazi Simba inaishi kifalme Rwanda.
Joyce Shedrack
July 24, 2026
Share :
Rais wa heshima wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘MO’ ameitoa timu hiyo katika hoteli iliyopewa na waandaaji wa Mashindano ya CECAFA Kagame Cuo na kuipeleka timu katika hoteli ya kisasa zaidi kwa gharama zake nchini humo.

Simba ipo nchini humo kushiriki michuano hiyo inayotarajiwa kuanza leo na kutamatika Agosti 07, huku Simba ikiwa miongoni mwa timu zinazoshiriki.
Wakati vilabu vingine shiriki vya michuano hiyo vikiendelea kukaa kwenye hoteli ambazo zinalipiwa na CECAFA, ni Simba waliokataa hoteli hizo na kwenda kwenye hoteli ya juu zaidi nchini humo.
Simba iliwajulisha CECAFA kwamba itafikia kwenye hoteli yenye hadhi ya juu zaidi na italipa gharama zote za ziada ili kuendana na hadhi na ukubwa wa klabu yao.
Simba imefikia hoteli ya nyota tano yenye hadhi ya juu zaidi jijini Kigali ya Mövenpick na gharama ya chini ya chumba ambacho kinatumiwa na staff wa Simba ni Tsh. 450,000 kwa siku moja ikihusisha chai ya asubuhi pekee.
Pia Simba imesafiri na chakula chake kutoka Tanzania ambacho itatumia muda wote ambao kikosi kitakuwepo nchini humo katika mashimdano hayo.
Viwango hivi vikubwa ni sehemu ya maelekezo ya Rais wa Klabu, Mohammed Dewji ambayo alitoa kwa Bodi ya kwamba kulingana na ukubwa wa taasisi kwa sasa basi kila timu inaposafiri basi chaguo la kwanza la hoteli ni lazima iwe na hadhi ya nyota tano.





