Mo Dewji akutana na Viongozi wa mtandao wa mashabiki wa Simba
Sisti Herman
July 14, 2024
Share :
Rais wa heshima na Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohammed Dewji leo amekutana na kufanya mazungumzo na Simba Executive Network (SEN).
SEN ni mtandao wa mashabiki wa Simba ambao huchangia ada ya 1,500,000 kwa mwaka kwa ajili ya miradi maalumu ya miundombinu ya klabu. Wanachama wa SEN hupata faida nyingi kama bima za maisha, tiketi za mechi na faida nyingine nyingi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi wa SEN akiwapo Mwenyekiti Abdulrazak Badru, Makamu wake Farouk Baghoza, Katibu Dkt. George Ruhago, Katibu Msaidizi Richard Mwalibwa na wanachama wa SEN. Menejimenti ya Simba iliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Imani Kajula.
Malengo ya Mwaka ya mtandao wa SEN ni kutengeneza uwanja wa mazoezi ili kuongeza idadi ya viwanja vya mazoezi Bunju.