pmbet

Mo Dewji alivaa mazima jambo la ujenzi wa uwanja wa Simba.

Joyce Shedrack

March 31, 2026
Share :

Mwekezaji na Rais wa heshima wa klabu ya Simba Mohamed Dewji amewasilisha barua ya Ujenzi wa uwanja wa Simba kwa Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo baada ya jopo la Watalaam kukamilisha mchoro wa mradi huo unaoitwa The Great Simba Project.
Mo Dewji aonyesha ramani ya uwanja wa Simba - PMTV
Taarifa kutoka kwenye Vyanzo vyetu ni kuwa Bilionea amewasilisha huyo amewasilisha barua hiyo kwa Bodi ya Wadhamini wa klabu ili waidhinishe ujenzi wa uwanja huo katika eneo la Bunju, Jijini Dar Es Salaam ambapo unatarajiwa kuanza mara moja.

Mradi huo ambao utahusisha Uwanja wa mpira wa miguu, viwanja vya mazoezi vya Kisasa, Hostel za Kisasa kwa ajili ya Senior Team, Wanawake na Vijana utaanza mara haraka iwezekanavyo baada ya Bodi ya Wadhamini kuidhinisha.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet