Mo Dewji ateta na viongozi wa klabu ya Simba
Eric Buyanza
April 15, 2024
Share :
Rais wa Heshima na Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amefanya kikao na viongozi wa klabu hiyo.
Kikao hicho, kimehudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa bodi wa klabu hiyo.
Kupitia kurasa zake za Instagram na X (zamani Twitter), Mo amesema kikao hicho kinaenda kuwa mwarobaini wa changamoto zilizopo klabuni humo.
“Nimefanya kikao na viongozi wa Simba SC kujua changamoto zipo wapi na namna ya kuzitatua. Kikao kimeenda vizuri,” ameandika.
Dewji amewaomba mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kutokufa moyo na kuendelea kushirikiana na kushikamana katika kipindi hiki ambacho klabu hiyo haifanyi vizuri.