Mo Dewji awashinikiza Wajumbe wa bodi Simba wajiuzulu, Try Again agoma
Sisti Herman
June 6, 2024
Share :
Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mfanyabiashara Mohamed Dewji ameripotiwa kutoa shinikizo la kujiuzulu nafasi zao kwa wajumbe wote aliowateua yeye ambapo mpaka sasa wajumbe watatu wamejiuzuli huku wengine watatu wakigoma.
Wajumbe waliojiuzulu ni pamoja na Rashid Shangazi ambaye pia ni Mbunge wa Mlalo na Hamza Johari ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mamlaka za viwanja vya ndege Tanzania huku mjumbe pekee aliyegoma kujiuzulu ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Salim Abdallah Muhene ‘Tryagain’.