Mo Dewji tajiri wa 12 Afrika
Sisti Herman
January 23, 2024
Share :
Jarida la Marekani la Forbes limetoa orodha ya 20 bora wa watu wenye ukwasi mkubwa zaidi Afrika huku mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji (Mo) akikwea mpaka nafasi ya 12 barani Afrika akipanda kutoka nafasi ya 15 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Utajiri wa Mo ambaye pia ndio bilionea kijana zaidi kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo umepanda kutoka Dola za Marekani 1.5 bilioni (Sh3.77 trilioni) mwaka uliopita hadi Dola 1.8 bilioni (Sh4.52 trilioni) jambo linalomfanya kuwa tajiri namba moja ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Kwingineko Rais wa CAF, Patrice Motsepe anakamata nafasi ya 10 akiwa na utajiri wa dola bilioni 2.7 huku mfanyabiashara, Aliko Dangote akishikilia usukani wa ukwasi Barani Afrika akiwa na utajiri wa dola milioni 13.9.
Ifuatayo ni orodha ya matajiri 20 Afrika ambao kwa mujibu wa Forbes utajiri wao umezingatia gharama halisi kwenye masoko ya mitaji na viwango vya kubadilishia fedha vilivyopo sokoni hadi Januari 8, 2024.
1. Aliko Dangote — $13.9bn (Manufacturing)
2. Johann Rupert & family — $10.1bn (Fashion & Retail)
3. Nicky Oppenheimer & family — $9.4bn (Metals & Mining)
4. Nassef Sawiris — $8.7bn (Construction & Engineering)
5. Mike Adenuga — $6.9bn (Diversified)
6. Abdulsamad Rabiu — $5.9bn (Diversified)
7. Naguib Sawiris — $3.8bn (Telecom)
8. Mohamed Mansour — $3.2bn (Diversified)
9. Koos Bekker — $2.7bn (Media & Entertainment)
10. Patrice Motsepe — $2.7bn (Metals & Mining)
11. Issad Rebrab & family — $2.5bn (Food & Beverage)
12. Mohammed Dewji – $1.8bn (Diversified)
13. Strive Masiyiwa — $1.8bn (Telecom)
14. Aziz Akhannouch & family — $1.7bn (Diversified)
15. Othman Benjelloun & family — $1.4bn (Finance & Investments)
16. Youssef Mansour — $1.3bn (Diversified)
17. Yasseen Mansour — $1.2bn (Diversified)
18. Christoffel Wiese — $1.2bn (Fashion & Retail)
19. Michiel Le Roux — $1.1bn (Finance & Investments)
20. Femi Otedola — $1.1bn (Energy)