pmbet

Mo Salah ampiku Gerrard kwa asisti Liverpool

Eric Buyanza

February 13, 2026
Share :

Mohamed Salah amempiku gwiji na nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard kwa kufikisha asisti 93 kwenye Ligi Kuu England ndani ya klabu hiyo.

 

Mo Salah alifikisha idadi hiyo ya asisti wakati alipomtengenezea bao pekee na la ushindi, Virgil van Dijk kwenye ushindi wa Jumatano usiku wa Liverpool wa 1-0 dhidi ya Sunderland.

 

Ryan Giggs anaongoza katika orodha ya wachezaji wenye asisti nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu England akiwa na 162, huku Kevin De Bruyne (119) akishika nafasi ya pili na Cesc Fabregas (111) akiwa nafasi ya tatu.

 

Wengine kwenye 10 bora ni Wayne Rooney (103), Frank Lampard (102), Dennis Bergkamp (94), David Silva (93), Mohamed Salah (93), Steven Gerrard (92) na James Milner (90).

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet